Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Saturday, September 17, 2011

HALI INAVYOENDELEA KUHUSU AJALI YA MELI ILIYOPELEKEA KUPOTEA KWA MAISHA YA WATU WENGI HUKO ZANZIBAR.

Meli ya MV Spice Islander ambayo ilipata ajali usikuwa wa kuamkia jumamosi juzi ya tarehe 10 imetuacha watanzania tukiwa kwenye majonzi mengi maana watu wengi wamepoteza maisha.Meli hiyo ilitengenezwa mwaka 1967.Ilitoka Ugiriki ikiitwa Mariana na baadae kuitwa Apostolos P na mwisho kuitwa Mv Spice Islander ilikuwa ishakuwa kuu kiukweli.Mpaka sasa idadi ya watu waliookolewa ni 620 japo inaenda ikibadilika badilika.Waliokufa 240 ambao miili imeonekana ambao miili haijaonekana 800.Idadi kamili ya waliokuwemo kwenye meli haiko wazi sana ila kwa majeruhi waliookoka na tukaongea nao kwenye kipindi wamesema kulikuwa na watu zaidi ya 2000.

Meli imeshazama kwenda chini kabisa urefu wa mita 400.Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa kwanza wa raisi anaeshughulikia maafa na muungano Mahamed Abood amesema tayari wataalamu kutoka Afrika kusini wamefika kutoa maiti zilizobaki huko kwenye meli kwa vifaa maalumu.

Watu waliopoteza ndugu jamaa na marafiki wakitambua miili ya ndugu zao kwa picha.



Watu wengi waliokoka kwa magodoro kama unavyoona pichani.Unaambiwa godoro zilisaidia sana maana godoro likiingia maji halizami linaelea.Wapo walioshikilia mifuko iliyojaa vile viatu vya yeboyebo na wao kuelea kwenye maji.Waliotumia matairi,milango ya mbao n.k kujiokoa.,

Imefahamika kuwa meli/boti nyingi hazina utaratibu wa kuelekeza abiria namna ya kutumia life jackets au hata kuwaonyesha zilipo.Wakati mwingine life jackets hizo zikiwa chache kulingana na idadi ya watu waliomo ndani ya chombo.Hata kama zipo ni za muda mrefu kiasi kwamba wapo wengi waliokufa kwa sababu life jackets walizovaa kuchanika baada ya kupigwa na mawimbi na wenyewe kuzama.
Kuna maswali mengi najiuliza mwenyewe hapa bila majibu.Hii meli nasikia ilikuwa ya mizigo kwa nini ilipakia abiria?Tena abiria wengi namna hiyo?ajali imeshatokea naamini waliofanya uzembe huo watawajibishwa kwa mujibu wa sheria lakini kama watanzania tunawajibika kufanya jambo litakalosaidia kwa siku zijazo.

No comments:

Post a Comment