Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Sunday, November 21, 2010

STOPAAAAAAAAAAA the legendary kufanya kazi na Dogo VJ ndani ya NOIZMEKAH chini ya D to the X kama anavyo sema shabang



Ni Jarome Frank a.k.a Stopa Rhymes the hip hop legendary kutoka street za fire tayari kasha achia songi la 'Na hustle' katika kazi hiyo amesimama na mzee wa kulalamika 'Rama D' na kwamba huo ni utambulisho wa albamu yake ya pili inayotarajiwa kuanguka kitaani hivi karibuni.

Kamaunakumbuka "Albamu yake ya kwanza iliitwa 'Shule ya Bure' na ilikuwa na ngoma kama 'Jiwe' aliyomshirikisha Nature, Staili tatu niliyosimama mwenyewe na nyingine kibao.
Sasa stopa kafanya kazi ya kushirikishwa na Dogo VJ ndani ya studios za Noizmekah Hapa hapa ARUSHA chini ya producer aliyeipeleka ARUSHA to the next level (DX),
dogo VJ anayesumbua pande za kaskazini na anayesemekana mkali zaidi ya YOUNG DEE.Dogo VJ mwenye track kadhaa zenye punch heavy aliyebaatika kufanya kazi na Mcs wakubwa kaskazini Mfano.Stopa,G nako(nako 2 nako),man batoo,toldo,DX,Finga luu,Donii, na wengine kibaooo. Hakika kazi aliyofanya na stopa ni balaa isake usikilize na ulinganishe punch.Inaitwa Afrika kwanza

Yereeeeeeee hatuwezi sema we are back!kwasababu ukweli ni kwamba we never left the building,nako 2 nako soldiers we battle hard



Nako 2 Nako soldiers 2mewavalia haters magwanda,na ni vita tu raundi hii",wasema machizi hawa wasanii wa hiphop wenye maskani yao pale ololoo a.k.a kaloleni Hapa hapa aruruu,na wamekamilisha video shoot ya track zao mbili chini ya kampuni ya Hoodpixx videos arusha,audio moja ikiwa ni "ndani ya nyumba" toka Bhitz na nyingine "kati kati" toka noizmekah pro arusha.kazi hizi zimetumia mazingira tofauti tofauti ya Atown,viwanja kama club AQ na Empire sports bar huku machizi na warembo kibao kuwapa support machiz wa "nako2nako" katika parts mbalimbali,video ya "kati kati" itatangulia kutimba media ikifatwa na "ndani ya nyumba" itayoachiwa mwezi baadaye,lord eyes asema "hatuwez ruhusu majembe yafie mahabusu,chama kubwa N2N sitakubali tu "kiseserere" hivi hivi (kuseserere-kuanguka)...na Gnako pia anawasisitizia washabiki wa n2n "kaeni macho kupata real ting'az toka kwa wakubwa wa kazi" huku Bou Nako a.k.a "ODINARI" awapa mashabiki na wadau wa hiphop uhakika wa vioo hivyo viwili walivyoshoot kutesa katika media kwa maana ni video mbili matata za madudez,makopo na mipini ya ukweli,huku anacheka,lord alimalizia kwa kusema "hatuwezi sema we are back!kwasababu ukweli ni kwamba we never left the building,nako 2 nako soldiers we battle hard!".