Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Monday, November 21, 2011

PRO24DJ ARUSHA TAKEOVER WALIVYOFUNGA MWAKA 2010 NDANI YA COLOBUS CLUB.

ULIKUWA ni usiku wa kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011 wakati wakali kutoka pande za Dar Pro24dj walipokuwa wakishambulia na kuwapa wakazi wa A-Town raha ambayo hawawezi kuisahau kamwe kwa kuporomosha muziki kabambe na uliopangiliwa kimataifa kutoka kwa madj wake matata bila kusahau wasanii mbalimbali kama JCB, Stopa na Nako2nako waliokonga nyoyo za mashabiki waliofika katika klabu ya Colobus.

Pichani hapo Dj Tassy anaonekana akijiandaa kuwasha fataki kuashiria kuukaribisha mwaka 2011.

Mamia ya watu wa mataifa mbalimbali walihudhuria tamasha la kuukaribisha mwaka mpya katika klabu Colobus wakisubiri kwa hamu fataki ziwashwe kuashiria kuukaribisha mwaka 2011.

Wasanii kuanzia picha ya juu JCB, Stopa na Nako2Nako walikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo katika picha hizo wanaonekana wakiimba kwa nyakati tofauti.

Crew nzima ya Pro24dj wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kitendo ambacho kiliwachanganya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo na kuwafanya kulipuka kwa furaha.

Mamia ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo wanaonekana wakiyarudi kwa nguvu ngoma kali zilizokuwa zikiporomoshwa na madj wa Pro24.

Baadhi ya Pro24djs wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto Dj Tassy, Dj Joe, Dj Arnold, Dj Chill na Dj John.

Lilikuwa ni tamasha lilihudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali pichani ni baadhi ya wazungu wakionekana kupagawa vilivyo na muziki uliokuwa ukipigwa na madj wa Pro24 katika tamasha hilo.

Pichani Dj Joe akiwa katika pozi na dadaz waliojitokeza katka tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment