Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Tuesday, January 17, 2012

DIAMOND CHUPU CHUPU KUHUKUMIWA MIEZI SITA JELA.......

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abduly Diamond,amekuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela mara baada ya kukutwa na kosa la kushambulia na kujeruhi,Mwandishi wa habari wa kujitegemea ambaye alitambulika kwa jina la Francis Godwin..Hatua hiyo imekuja mara baada ya Diamond pamoja na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya hakimu,na kuharibu Camera ya mwandishi huyo Desemba 31 mwaka jana,Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Hakimu Musua alisema kutokana na wote kukiri kosa alitoa hukumu ya kwenda jela miezi 6 au kulipa faini 50,000 na kumlipa mwandishi huyo 30,000.kila mmoja.Mwanamuziki huyo alifanikiwa kulipa faini hiyo,na kuachiwa huru yeye na wenzake.. 

Arifu haya ndio mojawapo ya MALAVIDAVI  KIZUNGUMKUTI..........

Uchumba wa klabu, usio na radhi ya wazazi kati ya ‘serengeti boy mpenda wakubwa’, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na staa wa kitambo Bongo, Wema Sepetu, umevunjwa rasmi.Mama wa Wema, Mariam Sepetu ndiye aliyeuvunja uchumba huo kwa msisitizo kwamba wakirudiana tena, basi kaburi lake halitakuwa ardhini bali mbinguni.Mariam amechoshwa na vitendo vya mkwe wa mtaani (Diamond), tabia yake ya kubadili wanawake kama abiria wa Dar wanavyokalia siti za daladala, imemfanya mama huyo kuapa kiapo kikali.“Sikufichi mwandishi, kwa kijana yule kurudiana na mwanangu haitawezekana kabisa. Simtaki huyo Diamond, alivyo na tabia yake havifai kuwa na mwanangu.“Mimi ni mzazi, Wema bado ni mtoto kwangu. Nilijua mapema uchumba wao hautadumu kwa sababu sikuwa radhi kwa hilo.“Walikutana huko na kuvalishana pete ya uchumba bila kufuata utaratibu,” alisema Mariam.
Mama huyo, akizungumza mbele mwandishi wetu, huku Wema akimsikia, alisisitiza: “Ninachojua ni kuwa mtoto wangu hawezi kurudi tena kwa huyo Diamond.“Siku ukiona amerudi, ujue maiti yangu itazikwa mbinguni lakini siyo ardhini.”
Kuhusu hatima ya mwanaye, Mariam alisema kuwa mpaka sasa hajapata mtu aliyemtolea posa, hivyo akaweka wazi kwamba akitokea aliye sahihi, hatasita kumkubali.
“Hajatokea mume hasa wa kumuoa Wema na moyo wangu ukaridhia, wanaokuja ndiyo hao kama huyo Diamond,” alisema.Amani limebaini kwamba Diamond hana tena nafasi kwa Wema, isipokuwa ‘dogo’ huyo aliyekulia Tandale, Dar, amekuwa akijipendekeza na kujitangaza kuwa bado wapo pamoja.
Katika shoo yake ya kuukaribisha mwaka 2012, iliyofanyika Januari Mosi, ndani ya New Maisha Club, Masaki, Dar, Diamond aliwadanganya mashabiki wake kuwa bado yupo na Wema.Diamond aliwapiga ‘changa’ mashabiki kuwa Wema ndiye usingizi wake, wakati mrembo aliyedaiwa kuchetuka naye, Jokate Mwegelo, alimtambulisha kwamba ni dada yake.Mbali na hilo, hivi karibuni, Diamond alimueleza ripota wetu kuwa yeye na Wema bado wapo pamoja.Alisema: “Hata sasa hivi nimetoka, nimemuacha nyumbani. Tumelala wote.Hata hivyo, katika maelezo yake, alikuwa anajikanyagakanyaga kuonesha anachosema kina walakini na ripota wetu alipofanya uchunguzi, alibaini kwamba Diamond hakusema kweli.Diamond na Wema, walianza uhusiano wao mapema mwaka uliopita.Oktoba Pili, 2011, Diamond alimvisha pete ya uchumba lakini wakati wa kukaribia kuuaga mwaka, alipigwa kibuti na mrembo huyo, ingawa anajaribu ‘kuuzuga’ ulimwengu kwamba bado wapo pamoja..

No comments:

Post a Comment