Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Tuesday, January 17, 2012

DIAMOND CHUPU CHUPU KUHUKUMIWA MIEZI SITA JELA.......

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abduly Diamond,amekuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela mara baada ya kukutwa na kosa la kushambulia na kujeruhi,Mwandishi wa habari wa kujitegemea ambaye alitambulika kwa jina la Francis Godwin..Hatua hiyo imekuja mara baada ya Diamond pamoja na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya hakimu,na kuharibu Camera ya mwandishi huyo Desemba 31 mwaka jana,Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Hakimu Musua alisema kutokana na wote kukiri kosa alitoa hukumu ya kwenda jela miezi 6 au kulipa faini 50,000 na kumlipa mwandishi huyo 30,000.kila mmoja.Mwanamuziki huyo alifanikiwa kulipa faini hiyo,na kuachiwa huru yeye na wenzake.. 

Arifu haya ndio mojawapo ya MALAVIDAVI  KIZUNGUMKUTI..........

Uchumba wa klabu, usio na radhi ya wazazi kati ya ‘serengeti boy mpenda wakubwa’, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na staa wa kitambo Bongo, Wema Sepetu, umevunjwa rasmi.Mama wa Wema, Mariam Sepetu ndiye aliyeuvunja uchumba huo kwa msisitizo kwamba wakirudiana tena, basi kaburi lake halitakuwa ardhini bali mbinguni.Mariam amechoshwa na vitendo vya mkwe wa mtaani (Diamond), tabia yake ya kubadili wanawake kama abiria wa Dar wanavyokalia siti za daladala, imemfanya mama huyo kuapa kiapo kikali.“Sikufichi mwandishi, kwa kijana yule kurudiana na mwanangu haitawezekana kabisa. Simtaki huyo Diamond, alivyo na tabia yake havifai kuwa na mwanangu.“Mimi ni mzazi, Wema bado ni mtoto kwangu. Nilijua mapema uchumba wao hautadumu kwa sababu sikuwa radhi kwa hilo.“Walikutana huko na kuvalishana pete ya uchumba bila kufuata utaratibu,” alisema Mariam.
Mama huyo, akizungumza mbele mwandishi wetu, huku Wema akimsikia, alisisitiza: “Ninachojua ni kuwa mtoto wangu hawezi kurudi tena kwa huyo Diamond.“Siku ukiona amerudi, ujue maiti yangu itazikwa mbinguni lakini siyo ardhini.”
Kuhusu hatima ya mwanaye, Mariam alisema kuwa mpaka sasa hajapata mtu aliyemtolea posa, hivyo akaweka wazi kwamba akitokea aliye sahihi, hatasita kumkubali.
“Hajatokea mume hasa wa kumuoa Wema na moyo wangu ukaridhia, wanaokuja ndiyo hao kama huyo Diamond,” alisema.Amani limebaini kwamba Diamond hana tena nafasi kwa Wema, isipokuwa ‘dogo’ huyo aliyekulia Tandale, Dar, amekuwa akijipendekeza na kujitangaza kuwa bado wapo pamoja.
Katika shoo yake ya kuukaribisha mwaka 2012, iliyofanyika Januari Mosi, ndani ya New Maisha Club, Masaki, Dar, Diamond aliwadanganya mashabiki wake kuwa bado yupo na Wema.Diamond aliwapiga ‘changa’ mashabiki kuwa Wema ndiye usingizi wake, wakati mrembo aliyedaiwa kuchetuka naye, Jokate Mwegelo, alimtambulisha kwamba ni dada yake.Mbali na hilo, hivi karibuni, Diamond alimueleza ripota wetu kuwa yeye na Wema bado wapo pamoja.Alisema: “Hata sasa hivi nimetoka, nimemuacha nyumbani. Tumelala wote.Hata hivyo, katika maelezo yake, alikuwa anajikanyagakanyaga kuonesha anachosema kina walakini na ripota wetu alipofanya uchunguzi, alibaini kwamba Diamond hakusema kweli.Diamond na Wema, walianza uhusiano wao mapema mwaka uliopita.Oktoba Pili, 2011, Diamond alimvisha pete ya uchumba lakini wakati wa kukaribia kuuaga mwaka, alipigwa kibuti na mrembo huyo, ingawa anajaribu ‘kuuzuga’ ulimwengu kwamba bado wapo pamoja..

Mamkwanja c ki2 arifu ila kuboresha life lawa SENEGAL ndio Mpango MZIMA........

Mwanamuziki mkongwe, mwenye heshima kubwa barani Afrika, Youssou N’dour, ametosa ulaji wa ubalozi wa watoto wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa ili apate nafasi ya kugombea urais. N’dour ambaye amekuwa balozi wa UNICEF kwa miaka mingi, amelazimika kuachana na kazi hiyo ili aweze kujikita kwenye mbio za kuwania Urais wa SENEGAL.Kwa mujibu wa taratibu za UNICEF, haitakiwi kwa mwanasiasa yeyote kufanya kazi za kibalozi chini ya mwavuli wa shirika hilo.

Vilevile, kwa mtu ambaye ni balozi wa UNICEF, pindi anapotaka kujihusisha na siasa, sheria zipo wazi kwamba ni lazima ajiuzulu wadhifa huo wa kijamii.Kutokana na sheria hiyo, N’dour amekubalia kuachia ulaji huo wa ubalozi na kushika siasa kwa maelezo kwamba anataka kufanya kazi kubwa ya kuwakomboa WaSenegal.Kazi ya mwisho aliyoifanya N’Dour chini ya UNICEF, ilikuwa Septemba 2011 alipokwenda Kambi ya Daabad, Kaskazini ya Kenya ambako alifanya shughuli za kuwasaidia waathirika wa njaa wapatao 435,000 kutoka Somalia.N’dour, alichaguliwa kuwa balozi wa UNICEF tangu Aprili 3, 1991, hivyo amefanya kazi za kibalozi kwa zaidi ya miaka 20.Uchaguzi Mkuu nchini Senegal, unatarajiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu na N’dour, anatabiriwa kuchuana vikali na rais wa sasa wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade...

CMB PREZOO AKATAA KUPATANISHWA NA JAGUAR...........

CMB Prezzo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake "For sure for shizzle, ameamua kuzungumzia Beef yake na Mwanamuziki ambaye na yeye anaendelea kuingiza mshiko kupitia ngoma yake inayokwenda kwa jina la KIGEUGEU Anajulikana kama Jaguar.kuhusina na swala zima la kupatanishwa ili kumaliza Tofauti zao , Prezzo amesema “nina bonge la saa ila sina time ya kuongea nae kwa sababu hana Adabu, yani hata KOFI ANNAN aje kutupatanisha, SITOKUBALI
Chanzo cha beef yao kilitokana na kauli nzito za JAGUAR zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ambazo amekua akiziendeleza kwamba PREZZO aache kujisifia kila siku kwenye media kuhusu kutupia bling bling, afanye muziki.kinachomkasirisha zaidi PREZZO ni kwamba, alieianza hiyo BEEF ni JAGUAR, na aliianza pasipo kuchokozwa na CMB, na wala haikuwa kutokea Prezzo akamkosea chochote JAGUAR hata kumsema vibaya.

MACHALII JAMBO SQUAD WADUMISHA MILA ZA KIMAASAI arifu.........

Machalii ya Ara a.k.a. Jambo squad watoto wa bibi wanafungua mwaka kwa kudrop kwaito jingine "Mamong'oo",Hili dude linazungumzia machalii wa kimasai na mitikasi ya town kwa hiyo ni idea flan comedy na kwa wakati huo huo kuelimisha jinsi gani kabila la wamaasai linadumisha mila,kimahadhi ni kwaito lilorekodiwa pande za noizmekah.com chini ya producer Defxtro na Machalii wa bibi waliopita katika pin ni Nigga C,Bam na Odinari."mashabiki wanatupa sana support na tunashukuru sana,pia ushirikiano tunaopata toka kwa Maproducer wetu Defxtro,John B,Dennis Mallya!Media zote pia zinazogonga pini zetu,Video ya disco malapa 2liyoishoot Grandmaster inamaliziwa na itatoka soon kwahivo wadau wakae mkao wa kubonya!...,

DULLY SYKES AFUNGUA STUDIO YA PILI HUKO TABATA.........


Mwanamuziki Dully Sykes afungua studio nyingine,Mambo yamemkalia pazuri staa wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully’ baada ya kufungua studio mpya ya kurekodi muziki.Studio hiyo aliyoipa jina la 4.12, ipo Tabata, Dar es Salaam na itakuwa ikirekodi aina zote za muziki.,Pamoja na matangazoStudio hiyo ni ya pili baada ya ile ya Dhahabu Records ambayo mwanamuziki huyo aliifungua zaidi ya miaka minne iliyopita.imeelezwa kuwa studio hiyo itafanya kazi kwa kujitegemea, ikiwa na maprodyuza wake wenye uwezo mkubwa.Imebainishwa kwamba kwa upande wake (Dully), atakuwa anapiga mzigo kwenye studio zote hizo kulingana na matakwa ya wateja wake...