Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Tuesday, January 17, 2012

DIAMOND CHUPU CHUPU KUHUKUMIWA MIEZI SITA JELA.......

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abduly Diamond,amekuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela mara baada ya kukutwa na kosa la kushambulia na kujeruhi,Mwandishi wa habari wa kujitegemea ambaye alitambulika kwa jina la Francis Godwin..Hatua hiyo imekuja mara baada ya Diamond pamoja na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya hakimu,na kuharibu Camera ya mwandishi huyo Desemba 31 mwaka jana,Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Hakimu Musua alisema kutokana na wote kukiri kosa alitoa hukumu ya kwenda jela miezi 6 au kulipa faini 50,000 na kumlipa mwandishi huyo 30,000.kila mmoja.Mwanamuziki huyo alifanikiwa kulipa faini hiyo,na kuachiwa huru yeye na wenzake.. 

Arifu haya ndio mojawapo ya MALAVIDAVI  KIZUNGUMKUTI..........

Uchumba wa klabu, usio na radhi ya wazazi kati ya ‘serengeti boy mpenda wakubwa’, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na staa wa kitambo Bongo, Wema Sepetu, umevunjwa rasmi.Mama wa Wema, Mariam Sepetu ndiye aliyeuvunja uchumba huo kwa msisitizo kwamba wakirudiana tena, basi kaburi lake halitakuwa ardhini bali mbinguni.Mariam amechoshwa na vitendo vya mkwe wa mtaani (Diamond), tabia yake ya kubadili wanawake kama abiria wa Dar wanavyokalia siti za daladala, imemfanya mama huyo kuapa kiapo kikali.“Sikufichi mwandishi, kwa kijana yule kurudiana na mwanangu haitawezekana kabisa. Simtaki huyo Diamond, alivyo na tabia yake havifai kuwa na mwanangu.“Mimi ni mzazi, Wema bado ni mtoto kwangu. Nilijua mapema uchumba wao hautadumu kwa sababu sikuwa radhi kwa hilo.“Walikutana huko na kuvalishana pete ya uchumba bila kufuata utaratibu,” alisema Mariam.
Mama huyo, akizungumza mbele mwandishi wetu, huku Wema akimsikia, alisisitiza: “Ninachojua ni kuwa mtoto wangu hawezi kurudi tena kwa huyo Diamond.“Siku ukiona amerudi, ujue maiti yangu itazikwa mbinguni lakini siyo ardhini.”
Kuhusu hatima ya mwanaye, Mariam alisema kuwa mpaka sasa hajapata mtu aliyemtolea posa, hivyo akaweka wazi kwamba akitokea aliye sahihi, hatasita kumkubali.
“Hajatokea mume hasa wa kumuoa Wema na moyo wangu ukaridhia, wanaokuja ndiyo hao kama huyo Diamond,” alisema.Amani limebaini kwamba Diamond hana tena nafasi kwa Wema, isipokuwa ‘dogo’ huyo aliyekulia Tandale, Dar, amekuwa akijipendekeza na kujitangaza kuwa bado wapo pamoja.
Katika shoo yake ya kuukaribisha mwaka 2012, iliyofanyika Januari Mosi, ndani ya New Maisha Club, Masaki, Dar, Diamond aliwadanganya mashabiki wake kuwa bado yupo na Wema.Diamond aliwapiga ‘changa’ mashabiki kuwa Wema ndiye usingizi wake, wakati mrembo aliyedaiwa kuchetuka naye, Jokate Mwegelo, alimtambulisha kwamba ni dada yake.Mbali na hilo, hivi karibuni, Diamond alimueleza ripota wetu kuwa yeye na Wema bado wapo pamoja.Alisema: “Hata sasa hivi nimetoka, nimemuacha nyumbani. Tumelala wote.Hata hivyo, katika maelezo yake, alikuwa anajikanyagakanyaga kuonesha anachosema kina walakini na ripota wetu alipofanya uchunguzi, alibaini kwamba Diamond hakusema kweli.Diamond na Wema, walianza uhusiano wao mapema mwaka uliopita.Oktoba Pili, 2011, Diamond alimvisha pete ya uchumba lakini wakati wa kukaribia kuuaga mwaka, alipigwa kibuti na mrembo huyo, ingawa anajaribu ‘kuuzuga’ ulimwengu kwamba bado wapo pamoja..

Mamkwanja c ki2 arifu ila kuboresha life lawa SENEGAL ndio Mpango MZIMA........

Mwanamuziki mkongwe, mwenye heshima kubwa barani Afrika, Youssou N’dour, ametosa ulaji wa ubalozi wa watoto wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa ili apate nafasi ya kugombea urais. N’dour ambaye amekuwa balozi wa UNICEF kwa miaka mingi, amelazimika kuachana na kazi hiyo ili aweze kujikita kwenye mbio za kuwania Urais wa SENEGAL.Kwa mujibu wa taratibu za UNICEF, haitakiwi kwa mwanasiasa yeyote kufanya kazi za kibalozi chini ya mwavuli wa shirika hilo.

Vilevile, kwa mtu ambaye ni balozi wa UNICEF, pindi anapotaka kujihusisha na siasa, sheria zipo wazi kwamba ni lazima ajiuzulu wadhifa huo wa kijamii.Kutokana na sheria hiyo, N’dour amekubalia kuachia ulaji huo wa ubalozi na kushika siasa kwa maelezo kwamba anataka kufanya kazi kubwa ya kuwakomboa WaSenegal.Kazi ya mwisho aliyoifanya N’Dour chini ya UNICEF, ilikuwa Septemba 2011 alipokwenda Kambi ya Daabad, Kaskazini ya Kenya ambako alifanya shughuli za kuwasaidia waathirika wa njaa wapatao 435,000 kutoka Somalia.N’dour, alichaguliwa kuwa balozi wa UNICEF tangu Aprili 3, 1991, hivyo amefanya kazi za kibalozi kwa zaidi ya miaka 20.Uchaguzi Mkuu nchini Senegal, unatarajiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu na N’dour, anatabiriwa kuchuana vikali na rais wa sasa wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade...

CMB PREZOO AKATAA KUPATANISHWA NA JAGUAR...........

CMB Prezzo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake "For sure for shizzle, ameamua kuzungumzia Beef yake na Mwanamuziki ambaye na yeye anaendelea kuingiza mshiko kupitia ngoma yake inayokwenda kwa jina la KIGEUGEU Anajulikana kama Jaguar.kuhusina na swala zima la kupatanishwa ili kumaliza Tofauti zao , Prezzo amesema “nina bonge la saa ila sina time ya kuongea nae kwa sababu hana Adabu, yani hata KOFI ANNAN aje kutupatanisha, SITOKUBALI
Chanzo cha beef yao kilitokana na kauli nzito za JAGUAR zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ambazo amekua akiziendeleza kwamba PREZZO aache kujisifia kila siku kwenye media kuhusu kutupia bling bling, afanye muziki.kinachomkasirisha zaidi PREZZO ni kwamba, alieianza hiyo BEEF ni JAGUAR, na aliianza pasipo kuchokozwa na CMB, na wala haikuwa kutokea Prezzo akamkosea chochote JAGUAR hata kumsema vibaya.

MACHALII JAMBO SQUAD WADUMISHA MILA ZA KIMAASAI arifu.........

Machalii ya Ara a.k.a. Jambo squad watoto wa bibi wanafungua mwaka kwa kudrop kwaito jingine "Mamong'oo",Hili dude linazungumzia machalii wa kimasai na mitikasi ya town kwa hiyo ni idea flan comedy na kwa wakati huo huo kuelimisha jinsi gani kabila la wamaasai linadumisha mila,kimahadhi ni kwaito lilorekodiwa pande za noizmekah.com chini ya producer Defxtro na Machalii wa bibi waliopita katika pin ni Nigga C,Bam na Odinari."mashabiki wanatupa sana support na tunashukuru sana,pia ushirikiano tunaopata toka kwa Maproducer wetu Defxtro,John B,Dennis Mallya!Media zote pia zinazogonga pini zetu,Video ya disco malapa 2liyoishoot Grandmaster inamaliziwa na itatoka soon kwahivo wadau wakae mkao wa kubonya!...,

DULLY SYKES AFUNGUA STUDIO YA PILI HUKO TABATA.........


Mwanamuziki Dully Sykes afungua studio nyingine,Mambo yamemkalia pazuri staa wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully’ baada ya kufungua studio mpya ya kurekodi muziki.Studio hiyo aliyoipa jina la 4.12, ipo Tabata, Dar es Salaam na itakuwa ikirekodi aina zote za muziki.,Pamoja na matangazoStudio hiyo ni ya pili baada ya ile ya Dhahabu Records ambayo mwanamuziki huyo aliifungua zaidi ya miaka minne iliyopita.imeelezwa kuwa studio hiyo itafanya kazi kwa kujitegemea, ikiwa na maprodyuza wake wenye uwezo mkubwa.Imebainishwa kwamba kwa upande wake (Dully), atakuwa anapiga mzigo kwenye studio zote hizo kulingana na matakwa ya wateja wake...

Monday, January 16, 2012

Mwanadada TigerEyes toka Arusha Tanzania......

Mwanadada TigerEyes toka hapa Ara-chuga anawaasa madem wote wanaofanya game wakaze buti mana yuko tight zaidi maelezo yani no mboyoyo hapa,"hakuna kulaza damu wala kusoundisha raia,niko serious sana na mziki chalaangu" asema nemy a.k.a TigerEyes mwanadafada anaye rap,kuimba na kudance katika crew la "NewKings" toka Arusha..."Noizmekah kwa dx ndo niliporekodia ngoma yangu hii ya "Grind on", beat ameunda producer Mosco ambae ameunda beat na vocal kasmamia bro dx mpaka ngoma kukamilika na kuwafikia wadau ma mashabiki zangu wote tanzania na dunia nzima,Sasa nakarbia kumaliza masomo ya chuo so nitakua full full hewani mithili ya noizmekah.com..Heshima tele ziende kwa Mungu kuniweka hai na my Mama kwa kunisuport katika muzik plus maproducer wangu kwa kuni guide na kunishauri...



HAMMY B WA B HITS ......KAMDISS JOH MAKINI KASEMA HANA SHUKRANI TATIZO NININI AISEEEE....



Baada ya kutoka kwa video mpya ya Joh Makini BYE BYE mmiliki wa studio ya B'Hits Hermer Tyrol Lyimo aka Hermy B amekuja juu na kuandika maneno hayo hapo chini kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Joh Makini You Have Officially Pissed Of B'Hits, Wimbo wa bye bye tulikupa bure baada ya kutujibu kwa dhihaka tulipodai malipo yetu, Hata kutupa Credit zetu kwenye video umeona kazi pia, ama kweli shukrani ya punda ni mateke, we mtu gani? Kumbuka ulipotoka!!! Kumbuka Enzi za Magic Fm!!!

Producer Mosco wa PYG Majengo pande za ARA..................


Machalii ya ArA Ndugu pacha na Jambo squad wanaofahamika zaidi kama MAALMANDO,wanakuja na pini brand new la "RAKATA" ikiwa ni genre ya kwaito-mdundix ikiwa ni brand new style mojawapo wanayokuja nayo machizi hawa wenye maskani yao pande za arachuga mtaa wa cheka na mecca!Ngoma tumerekodi kwa Defxtro a.k.a DX pande za noizmekah.com juu ya beat la producer Mosco wa PYG Majengo apa apa pande za ARA,Maalmando tunawaahidi fans wetu mwendelezo mnene katika muziki huu mwaka 2012 na mpango mzima ni hela so tuendeleze hasoling kusakanya dinari arif...oooooooi MEKACHEKA Style 4LIFE....
Rakatatata (Mosco.NOIZ).............
MAALMANDO toka Arachugga na pin brand new "RAKATA".......

Sunday, January 15, 2012

Lady fire toka Jambo Squad na "sidanganyiki"



Ladyfire,Msanii wa kike katika fani ya hiphop anakuja na "sidanganyiki",pini la kuwakandia mafataki na tabia zao chaf za kurubuni wasichana wa shule.Akiwa kama Hiphop mc wa kike from arachuga,lady fire anawaasa wenzake kuwa makini sana maana maisha hayajirudii,"kila mmoja anapaswa kujua kwamba mafataki wanachangia sana katika kuwaharibia madem wengi maisha,ndio mana kupitia nyimbo ii nlorekodi pande za noizmekah.com nimecheza nafasi ya msichana asedanganyika.much love kwa ma brothers wote from Jambo squad kwa kunipa shavu hili na producer wangu na mashabiki zangu wote,nawapendaga sana aseeeeeeee..........

NiggaC toka jambo squad awapa fasi vatoloco the red ku-ngastuka!!



Mtoto wa bibi a.k.a. chalii chaplin a.k.a. mong'oo inchaji vema zaidi kama niggaC toka Jambo squadere sedere bidengere biae full papi haina manjota kwa fas mpaka mbulu kwa mama lulu tam kk mtori sio chungu ka ngorotii anakam tena round ii kwa kishindo na machiz wa vatoloco the red a.k.a ka kang kang!..ndani ya remix version ya track ya "ngastuka" ambayo imerekodiwa chini ya producer dx a.k.a defxtro pande za noizmekah.com arusha,'Humu ndani kama kawaida 2mewachana maraia viongozi wa nchi wanaofisidi na kutuuza asee,ni full machungu na hatuachi kuwalalamikia mpaka mabadiliko ya ukweli yaje!ooooooooooooooiiii

GhettoDiva anahitaji Boy!!!!!

Rappa Ghettodiva a.k.a. GHeTtODiDiz anafungua mwaka kwa kusema "Need A Boy",Ngoma inayozungumzia jinsi gani manzi hardcore anataka mchizi wake,yaani boyfriend awe,Ghettodiva akiwa ni msanii rappa wa kike mwenye maskani yake pande za Arachuga,asema "Nafaham title ya track ina kautata flan but its exactly what me n ma producer thought would fit best ayo mashairi apo ndani so much love to ma producer pande za noizmekah.com,my family including "Junior" and all ma fanz,katika game y'all are ma family and bila ninyi hakuna mimi,otherwise mbali na hii single niloachia,natarajia kutembelea nchi jirani ya Kenya kufanya kazi na wasanii wa kule katika kukuza career yangu!

Ghettodiva a.k.a GeRoDidiz aja na DICTATION........


Ghetto diva asema "u gatta pay attention to this,hizi flow zafanya watu wadata na dictation zangu dunia nzima zatanda so write it down! "nimerecord ii track juu ya beat ya producer mosco wa majengo arusha,vocals kasimamia defxtro pande za noizmekah.com na mixing so ma fans wote wa hiphop wajue GD bado niko hai kimziki ni mkimbizano na maisha hapa na pale tuko pamoko,shout out kwa mahomiez freelodaz pande za masaki,media personel zote TZ na EastAfrica kiujumla i Love y'All...

Moplus na Tshirt za "MoveMent".........



Hiphop MC Moplus,baada ya kuachia ngoma ya "movement" alowashirikisha Adomido pamoja na SlimDizzy,Ngomailopokelewa vema tu katika media kadhaa nchini,sasa amewapa nafasi mashabiki zake wote kunyuka Tshirt za "MoveMent" kwa elf kumi tu!!!!'asema "Project zangu za kimziki nazifanya kwakuwashirikisha wadau na mashabiki zangu ambao kwa ujumla ndio jamii kwa pamoja,I love ma people coz they Love me!Much love kwa Vinega juzkati kutupa burudani katika Antivirus show,nilijifunza kwamba Artists/Mcs especially wa hapa arusha tunatakiwa kuungana na kufanya kazi kwasababu maslahi yapo sana,ni nidhamu na bidii imekaa kushoto otherwise we all get support from our fans,radio zisitudalalie wala kutugawa,join the movement!!!MUZIKI UNALIPA...

AdoraboMc ft Mosco & Moplus-Oh Life.......


AdoraboMc,msanii wa hiphop toka arusha pande za ungalimited,ambaye pia yumo katika kundi la mgombaz niggaz anakuja na new pini aloipa jina "oh life",humu ndani kawashirikisha Mosco & Moplus,Ikiwa ni project single ya kuukaribisha mwaka 2012,ngoma hii tumezungumzia maisha ki concious zaidi,Mosco kanyonga beat na vocal mixing kasmama Defxtro.Holla to all ma fans,maproject yatayofata baada ya hii ngoma ni pamoja na "Next step" ambayo pia tumegongea pande za noizmekah.com...