Deejay_Ezecking ..............

2 getha we can do more................

Wednesday, November 23, 2011

MARK MUSHI WA ITALY... Msanii na Prodyuza anayepania kuja kuwafuta machozi wasanii Bongo!!

Maliki Mushi aka Mark.Mushi wa Italy ambaye ni msanii anayepiga mishe zake huko Italy huku akiendelea na mafunzo yake ya U-Prodyuza amesema anakuja Bongo kuwashika, akiwasiliana kwa karibu sana ya blog yake hii ya deejayezecking, Mark anakuja Bongo kufungua bonge ya Studio itakayokwenda kwa jina la MARANGU RECORDS ambapo inaonekana maskani yake kubwa kuwa pande za A Town.



Mark tayari amesha record single yake inayoitwa "Futeni machozi". Ktk Single hiyo aliyoifanyia Italy Mark amewaasa wasanii wa mziki hasa wa Bongofleva kufuta machozi kwani mkombozi wao anakuja na atasikiliza kilio chao.
Pia Mark anaonekana kuhusudu sana kazi zinazofanywa na Marco Chali, so mdau tutegemee mikono mikali sana ya level zilezile kutoka kwa Prodyuza mpya wa Marangu Recordz Mark Muitalianooooooo

Mark akiwa ktk pozi nchini Italia.
blog yako ya deejayezecking itaendelea kuwaletea picha za matukio mbalimbali ya Mark Muitaliano ktk pozi, hivi karibuni.

Monday, November 21, 2011

UKICHEZA KIDUKU UTAKUA SHOGA BAADA YA MIAKA 40 TAKE CARE....






INASEMEKANA: SO TAKE CARE NA UJIULIZE
KUTOKA KWA WATAALAMU WA MICHEZO YA DANCE WAMETOA MADHARA YATAKAYO LETWA NA MCHEZO WAKIDUKU KWA WANAOCHEZA WOTE PINDI WATAKAPO FIKIA UMRI AMBAO HAURUHUSU KUCHEZA NA KUWALAZIMU WAO KUSHIKWA NAMATAMANIO SEHEMU ZA NYUMA KWANI MCHEZO HUU UNALEGEZA SEHEMU ZA MAKALIO NA KUKUSABABISHIA WEWE HAMU PINDI UTAKAPO ACHA KUUCHEZA NA KUKUSABABISHIA WEWE KUA SHOGA. KWAHIYO MCHEZO HUU SIO MZURI KWA WANAUME.KWANI UTAKAPO ZEEKA UTAKUSUMBUA HIZO NITETESI ZILIZOPO MTAANI KUHUSU MCHEZO HUO SO ANGALIENI SANA NYIE MNAO CHEZA MCHEZO HUO KWANI INASEMEKANA SOUTH AFRICA WATU KADHAA WAMESHA SHIKWA NA GONJWA HILO LA UDUKU(ZIDUKU KISOUTH.PIA WATU KADHAA WAMESEMA MCHEZOHUO UNA SISIMU ASANA SEHEMU ZA NYUMA UNAPO CHEZA KAMA HUAMINI JARIBU HII NI TETESI YA TAHADHARIIIII.

NAKO2NAKO WAKERA MASELA HAPA A TOWN....MAUDHAIFU YA N2N KUTOKA KWA MASELA..HAYO HAPO CHIN SOMA...NA YASEMEKANA VATOLOCO TEGEMEO LA HIP HOP ARUSHA.





yasemekana badala ya nako 2 nako kushindwa kuiwakilisha arusha ki hip hop machizi wa mtaani wamesema kwasasa wamekubali kua mavato kwasababu nako imesambaratika kutokana na kutofautiana kiarakati,ambapo masela wamesema hawafurahishwi na vitu vifuatavyo kutoka kwa n2n, kuwashobokea wabongo na mademu na kusababisha kutofanya kazi kikamilifu,kusujudia ma dj na watangazaji,kuto saidia underground,kushoboka kufanya featuring na mc wa bongo fleva,mcz wadogo wamejiuliza kwanini watolewe na mabongofleva wakati wao ndio walitakiwa wawa bebe mfano dogo janja katolewa na tip top wakati nako walikua na nafasi kubwa ya kumtoa,wameusaau uArusha,wamesaliti geto, wanajifanya hip hop kumbe mabongo fleva, pia masela wamesema fananisha nyimbo ya ndio zetu na nyimbo nyingine zinazo toka sasa ndipo utaona jinsi hawa machizi walivyo kua masoro,pia wanamkubali IBRA da husla kwani wamesema wana hisi yeye ndiye alikua hip hop kwa sana katika kundi lile wamesema fananisha vato na nako kwa sasa alafu useme nani hip hop? .pia wamesema wanasikitishwa sana na G nako kua mziba kiraka wa Joh makini pindi anapokua kazini na kumfananisha na......."neno limezuiliwa kwaajili ya kupunguza makali". hicho ndio kilio cha masela juu ya nako2nako ...selaa mmoja kaskauri BU nako aame nako 2 nako hiyo sio sehemu yake,,,..nimtazamo tuu wa masela.................
Arachuga hip hop drink..................

PRO24DJS.

Hawa ni wakali wa kuwaburudisha wale wote wapendao burudani ya music na kwasasa wameuva mia mkoa wa Iringa katika Club VIP ni noumaah!!!
Hapa ni kazi mbili kwa wakati mmoja ni noumaah!!! (kushoto) ni Dj Arnold na anayefuata ni Peter moe


Wote mnakaribishwa....!!!!!

PRO24DJ ARUSHA TAKEOVER WALIVYOFUNGA MWAKA 2010 NDANI YA COLOBUS CLUB.

ULIKUWA ni usiku wa kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011 wakati wakali kutoka pande za Dar Pro24dj walipokuwa wakishambulia na kuwapa wakazi wa A-Town raha ambayo hawawezi kuisahau kamwe kwa kuporomosha muziki kabambe na uliopangiliwa kimataifa kutoka kwa madj wake matata bila kusahau wasanii mbalimbali kama JCB, Stopa na Nako2nako waliokonga nyoyo za mashabiki waliofika katika klabu ya Colobus.

Pichani hapo Dj Tassy anaonekana akijiandaa kuwasha fataki kuashiria kuukaribisha mwaka 2011.

Mamia ya watu wa mataifa mbalimbali walihudhuria tamasha la kuukaribisha mwaka mpya katika klabu Colobus wakisubiri kwa hamu fataki ziwashwe kuashiria kuukaribisha mwaka 2011.

Wasanii kuanzia picha ya juu JCB, Stopa na Nako2Nako walikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo katika picha hizo wanaonekana wakiimba kwa nyakati tofauti.

Crew nzima ya Pro24dj wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kitendo ambacho kiliwachanganya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo na kuwafanya kulipuka kwa furaha.

Mamia ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo wanaonekana wakiyarudi kwa nguvu ngoma kali zilizokuwa zikiporomoshwa na madj wa Pro24.

Baadhi ya Pro24djs wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto Dj Tassy, Dj Joe, Dj Arnold, Dj Chill na Dj John.

Lilikuwa ni tamasha lilihudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali pichani ni baadhi ya wazungu wakionekana kupagawa vilivyo na muziki uliokuwa ukipigwa na madj wa Pro24 katika tamasha hilo.

Pichani Dj Joe akiwa katika pozi na dadaz waliojitokeza katka tamasha hilo.

Mavi2ziiii ya PRO-24 DJS...........

Wakati Watanzania wengi wameanza kupata mwamko na idadi ya watu kuongezeka kutoka nyakati za usiku katika kumbi mbal;i mbali za starehe,vijana wa pro-24 dj wamejidhatiti kwa ajili ya kukata kiu kwa watu ote ama wadau wa burududani nyakati zote usiku na mchana..

Ni vijana ambao naweza sema gumzo hv sasa hapa Tanzania kwanza ni vijana ambao wanajua mziki nini na wanajua mdau wa muziki anataka nini..na wakati gani..
                                    Mdau akiwa amejipatia zawadi kutoka kwa pro24djs

Kwanza style ya upigani wao muziki ni tofauti kabisa,aina ya vyombo wanavyotumia ni vya kisasa kabisa..

kutana nao kila Jumatano pale masai club...kuanzia saa 3 hadi kukuche Alhamisi kutana na Club Billicanas kuanzia saa 3 usiku hadi uchoke wewe mwenyewe maana ni usiku wa akina dada..kutana na dj tass naye anaporomosha ngoma ndani ya savannah lounge & bar ambapo kila mdau wa burudani anajua na si swali kabisaaa...kwa wakazi wa arusha kutana nao pale via via kwenye saturday night fever,hapa utapata techno,house,dance,kwaito,r&b - hip hop,na nyingine kibao usikoe uhondoo huuu...

Kutana na mzee mwenye ugonjwa wa ajabu,anayepigana wanawe wasije ishia alipo yeye.



Chandra Wisnu, 57, anasemekana kuwani  mmoja wa watu waliowahi kupata ugonjwa wa ngozi mbaya kuliko mtu mwingine yeyote hapa duniani.
Mzee huyu raia wa Indonesia,ni mara chache sana hutoka nyumba yake, na mara inapombidi kutoka hujitahidi kufunika uso wake pamoja na miwani ili kuepusha kuwa kituko njiani .Ilianza kama  kipele kimoja wakatii ana umri wa miaka 19,alipofkisha umri wa miaka 24 vipele vilikuwa vimetapakaa karibu sehemu yote ya mgongo wake,By the time ana umri wa miaka 32 tayari vipele vilikuwa vimefunika mwili wake wote
Alijaribu kuwaona madaktari mbalimbali lakini hakuweza pata tiba ya ugonjwa wake,aliambiwa tatizo lake ni la kurithi na isingekuwa rahisi kupata tiba yake.Baada ya kushindwa himili mzigo wa gharama za matibabu mzee huyu alilazimika kuishi maisha ambayo hakuna mwanadamu ambaye anaweza penda ishi hata kwa malipo ya kiasi gani.

Alisema “Hapakuwa na  special treatment katika kipindi chote hiki nnachoumwa, nlikuwa tu naambiwa nenda hapa nenda pale”
“Baada ya hali kuwa mbaya baba hakuona tena point ya kuwa ananipeleka tena hospitali,na tangia kipindi hiko sijamuona tena daktari”
“Huu ugonjwa una athari kubwa katika maisha yangu,hivi vipele huwa vina washa kupita maelezo kipindi cha joto”
“kupunguza muwasho na kuepusha watu nicheka huwa navaa majacket matatu na kufunika kichwa changu
“Hamna mtu aliyewahi nidhihaki directly but huwa wananiangalia sana na kunikwepa,watu wengi huwa wana behave very strangely kila wanaponiona
“Sio siri inanifanya nisiwe na amani,na wakati mwingine huwa nashikwa na hasira”
“Wengi hwa wanaogopa sura yangu na pia hukwepa nisiwaambukize”
“Kwa sababu hiyo,ni mara chache sana kuniona natoka nje,na nikitoka basi huwa nakwenda kumpick binti yangu shuleni,na mara zote nikienda huwa nafunika uso wangu pamoja na kichwa ili rafiki wa mtoto wangu wasiwe wanamcheka mwanangu kwamba ana baba mwenye sura ya ajabu”
Nanik Tri Haryani,mke wa huyu mzee,33, anasema: “Zamani sana wakati huu ugonjwa unamuanza mume wangu kutokana na muonekano wake kuwa mbaya aliniomba niondoke na kumwacha peke yake na kamwe nisirudi”
“Nilikataa. kumuona mwenzangu anapitia kipindi kigumu kama hiki katika maisha na kusimama pamoja naye kwangu mimi niliona ni ishara ya nguvu na sio udhaifu”
Leo hii mzee Chandra ameamua kutojificha tena na kujitokeza mbele ya dunia akipiga magoti na kuomba kama kuna mtu anaweza wasaidia wanae wawili,Martin,32,na Lis,26,ambao nao wameanza onesha dalili ya kupata ugonjwa huu unaomtesa baba yao
Mzee huyu hana uwezo wa kuwapeleka wanae kwa daktari na hofu yake kubwa ni kwamba wataishia kuwa na muonekano kama alionao
Alisema: “sijawahi wapeleka hospitali,kwani ni ghali mnoo,na sina uwezo”
“Kama patatokea nafasi ya kupata matibabu ya bure,sita sita kuitumia hiyo nafasi ila kwa sasa sina kingine nnachohitaji maishani zaidi ya matibu kwa familia yangu”

Yaliyojiri Epiq Nation MTWARA..............

 Mwasiti

Kiduku kinapokubali

 Rais wa Masharobaro

 Suma

 Prof Jay

 Roma

Mackay

Monday, November 14, 2011

nYeUc Tiiiiiiiiiiii................................

  Weusi Kampuni?????? G Warawara da City Finest, Joh Makini Mwamba wa Kaskazini, Bonta Conscious, & Lord Eyez with Good Music Family (G.M.F).............................